KWANINI WATAYARISHAJI WA FILAMU WALIO NA VIPAJI NI MARA CHACHE SANA KUFANIKIWA NA HII INATOKANA NA HAYA

WATAYARISHAJI WAFILAMU WALIO NA VIPAJI NI MARA CHACHE SANA KUFANIKIWA NA HII INATOKANA NA HAYA

Katika kufanikisha ndo yako ya utayarishaji wa filamu kwenye dunia hii,Kipaji hakiko sawa na mafanikio, hivyo kuna sababu nyingi tofautitofauti zinazopelekea mafanikio ya mtu, aidha wazazi wako wawe matajiri ama kuwepo na Connections/miunganisho katika tasnia. Lakini tofauti na hapo utalazimika kufanya kazi kwa bidii, na hakuna mtu mwenye atakupa chochote. Acha kusubiri ruhusa na badala yake nenda nje na uonyeshe filamu zako mwenyewe kwa uwezo wako. Anza kujifunza biashara za filamu na kwenda nje na kufanya ili uweze kuoneka kupitia kazi zako mwenyewe. Hivyo basi, kufanya bidii kunashinda kipaji/ talanta pale kipaji kinaposhindwa.

Unapohitaji mafanikio katika tasnia hii ya filamu inakupasa kujitambua wewe mwenye, kwa maana ya kuwa wewe ni nani? pia kutambua thamani ya unachokifanya. Hapa swala zima linaloweza kupelekea mafanikio katika tasnia hii ni wewe binafsi kusimama na kujiamini ukiona kuwa unaweza fanya bila ya mtu yeyote kukuzuia aidha kwa kukukatisha tamaa, maana wanasema "Siku zote kwenye maisha hakukosi Changamoto, changamoto zipo tu ila ukizihofia ndipo unapozipatia uzito". Na hii unahitajika kuwa na msukumo wa ndani ambao haku mtu yeyote atakayeweza kukuzuia ama kukukatisha tamaa kwa lengo la kukurudisha nyuma ili ushindwe kuendelea.

Hivyo basi katika njia ya kufikia mafanikio kwenye tasnia ya filamu inakubidi kujitoa kwa hali na mali panapohitajika, pia kwa kuweka nia thabiti huku ukipangilia mipango yako iende sawaswa na wewwe utakavyokuwa umeipangilia kwa ufasaha, hapa utakuwa umeanza kuujenga msingi wa mafanikio yako. Mambo ya msingi kabisa ni kujiamini mwenyewewe kwa kuchukua hatua ya kufanya uthubutu wa kufanya kile unachokihitaji na unachokipenda pia ambacho unakiona kitaweza kukunufaisha kwa kukuingizia pesa kwenye maisha yako. Siku zote kwenye njia ya kufikia mafaniki hapakoswi mawe ambayo utajikwa ila hiyo isiwe ni kikwazo cha wewe kusitisha safari yako ya mafanikio. maana wanasema unapojihisi kukata tamaa ndipo "mafanikio yanapoanza". KWAHIYO KIKUBWA NI USHIRIKIANO NA KUFANYA KAZI KAMA TIMU HAPO TUTAFIKA.

"Juhudi zako binafsi ndizo zitakazo kupjengea msingi wako na kukupeleka kwenye mafanikio unayoyahitaji katika tasnia ya filamu"

Written By
Director Bony Tz
+255 0759 142 565
boniphacemathias852@gmail.com
Zaidi, tembelea tovuti yetu: TON GEN PRODUCTION


Post a Comment

Please You can Follow Us through Subscribe or click follow

أحدث أقدم