Mambo Sita(6) ya msingi katika kandaa "low Budget film"/ kuandaa filamu kwa bajeti ndogo

 

MAMBO SITA(6) YA MSINGI KATIKA KUANDAA FILAMU YA BAJETI NDOGO/LOW BUDGET FILM

1.      Punguza idadi ya maeneo/locations

Hili ni jambo ambalo linafanyika katika hatua mbili, wakati wa kuandika script kwa maana ya mwandishi wa script atakuwa anafahamu ni maeneo gani hiyo filamu itachukuliwa/ shooting itafanyikia, pia inatokea baada ya script kuwa tayari ishaandikwa na ipo kwa mwongozaji/director husika aliyepewa jukumu la kuisimamia filamu hiyo. Hivyo yeye ndiye atachagua ni maeneo gani hiyo filamu itachukuliwa. Hivyo basi ili kupunguza gharama za usafiri, kulipia hayo maeneo pamoja na vyakula inabidi kupunguza idadi ya maeneo ili kuweza kuandaa filamu kwa bajeti ndogo au ya kawaida. 


2.      Weka kiwango cha chini cha wahusika

Pia jambo linguine la msingi unapohitaji kuandaa filamu yako kwa katika Bajeti ndogo, unahitajika kupunguza au kuwa na idadi ndogo ya wahusika katika stori/script yako. Hili jambo linafanyika hasa kabla ya kuandika script ila hata kama imeandikwa basi itabidi ilekebishwe kwa kufanyiwa uhariri na kuanza kupunguza idadi ya wahusika jambo ambalo linaweza kuingiza gharama kubwa ya kufanya malipo kwa wachezaji au waigizaji. Ikiwa na maana ya kuwapatia huduma mbalimbali, vifaa vya kazia, kama vile mavazi, na mahitaji mengine yatakayohitajika ili kumbeba mhusika yeyote katika scene. Hivyo kuepuka gharama kubwa na ili uweze kumudu kutayarisha filamu ya bajeti ndogo inabidi kuwa na idadi/ kiwango cha chini cha wahusika. 


3.      Andika stori ambayo inahusu wakati uliopo

Jambo linguine katika kufanikiwa kuandaa filamu kwa kiwango kidogo cha fedha kwa maana ya “low Budget Film” , inakubidi kufanya uamuzi sahihi kabla ya kuiandika stori yako. Uamuzi huu ni kuepuka stori zinazohusu wakati uliopita, mfano “maisha ya mhusika wako akiwa mdogo au kipindi yupo shule anasoma”. Ukifanya hivi itakusaidia kuepukana na gharama zingine zisizo za msingi endapo unahitaji kuandaa filamu kwa kiasi kidogo cha fedha na hakika utafanikiwa. 


4.      Epuka kuweka Special effects, stunts na Make up effects.

Pia unapoiandaa script yako kwa malengo na makusudio ya kutayarisha filamu kwa bajeti ndogo, inakubidi, kupunguza ama kutokuweka kabisa Special effects, ambazo hufanyika wakati wa kutayarisha filamu/ wakati wa “production”, ikiwa na maana ya “location”. Mfano wa hizo “special effects” ni kama vile “kemikali au michanganyo inayotumika kumwanda mtu aliyeungua kwa ajali ya moto kwa kumtengenezea majeraha usoni ionekane kama uhalisia, pia baadhi ya vitu vingine ambavyo vitahitajika kwaajili ya muigizaji kuvitumia wakati akicheza nazo ni sehemu ya special effects kwa maana ya Props kama vile chakula, jiko, silaha, gari, n.k. Vyote hivyo visipotumika kwa kiasi kikubwa au kutotumiwa kabisa itawezesha kuandaa filamu kwa Bajeti ndogo. 


5.      Epuka/epuka scene za usiku

Hili jambo nalo linafanyika Zaidi wakati wa kuandika script na wakati wa kutayarisha filamu kwa maana ya “production”. Hapa anahusika mwandishi wa mswaada au “script” kutokuweka scene za usiku wakati anaandika, pia kwa upande mwingine director/mwongozaji naye anajukumu hili la kubadili scene kwenye script ambazo zilitakiwa kuchezwa usiku ziweze kuwa ni scene zitakazochezwa mchana, hapa director atafanya kitu kinaitwa script break down kabla ya kufanya shooting ili kubadili hizo scene za usiku na kuwa za mchana.

Kujua Zaidi tazama video kwenye hii: https://youtu.be/W5lCJ_lMEUQ

Imeandaliwa na Director Bony/ Boniphace Mathias Miloha

Wasiliana nasi: 0759142565

Tembela tovuti yetu: https://tongenproduction.blogspot.com

 

------Have a nice learning-----

Post a Comment

Please You can Follow Us through Subscribe or click follow

أحدث أقدم